Changamoto ya mimba za utotoni umesababisha zaidi ya wanafunzi 1000 wamekatisha masomo mkoani Mwanza katika kipindi cha miaka mitatu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna amesema kuwa takwimu hizo ni zile zilizotolewa taarifa kwenye madawati ya jinsia ya polisi.
Kamanda wa polisi anasema kuwa takwimu hizo zinaashiria tatizo la mimba linaendelea kuathiri jamii hususan watoto wa kike. Mkurugenzi wa shirika la Kivulini Yasini Ally amesema kuwa changamoto kubwa ambayo inaikumba jamii kwa hivi sasa ipo kwenye malezi ya watoto na kusababisha baadhi ya watoto kujitumbukiza kwenye mahusiano yasiyo salama.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kuweka mikakati wa namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa waathirika wa vitendo vya ukatili mkoani Mwanza wametoa rai kwa wadau kushirikiana
Wadau kikao hicho kimewashirikisha waandishi wa habari,madaktari, polisi na maafisa maendeleo ya jamii kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa mwanza.