Star Tv

Wakulima 170 wa kitongoji cha Lyahamile Mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa  wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wameachwa njia panda baada ya serikali ya wilaya hiyo kuwapiga marufuku kuendelea na shughuli za kilimo katika shamba la Mpunga la Katenge kwa madai kuwa eneo la Shamba hilo lina mgogoro.

Add a comment

 Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la  “Mfalme Zumaridi” lililoko mtaa wa Iseni kata ya Butimba hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.

Add a comment

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu wa Gereza baada ya msamaha uliotangazwa na Rais Dk John Magufuli.

Add a comment

 

Wasomi na wahitimu wa elimu ya juu nchini, wameshauriwa kuwa wabunifu na kuachana na kasumba ya kuchagua kazi za kufanya ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ajira.

Add a comment

KESI ZA UHUJUMU UCHUMI; Washtakiwa waanza kukiri makosa Washtakiwa watano wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwemo wakili, Dk Ringo Tenga wamemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuomba kukiri makosa yao, ambapo wanadaiwa kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya bilioni nane Wakili wa washtakiwa hao, Byrson Shayo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Add a comment

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa rais wa kwanza wa Tanganyika ambaye aliaga dunia mnamo mwaka 1999.

Hii leo Hayati baba wa Taifa akitimiza miaka 20 tangu kutokea kwa kifo chake. Maadhimisho ya muasisi wa Taifa la Tanzania yamefanyikia Kitaifa mkoani Lindi. Hayati Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Mkoani Mara, nchini Tanzania.

Hayati  Nyerere  anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.

 

Add a comment

Watu wenye Ualbino mkoani Mara wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa mafuta maalumu wanayotumia kupakaa ngozi zao ili kuepusha vidonda na michubuko ya ngozi inayosababishwa na mionzi ya jua hali inayopelekea baadhi yao kukumbwa na magongwa ya saratani ya ngozi.

Add a comment

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani Misungwi mkoani Mwanza ili kupisha uchunguzi wa mgogoro uliojitokeza baina ya kikundi cha Mlimani ambao ni waanzilishi wa uchimbaji, mmiliki wa shamba na  mwekezaji mpya aliyejitokeza kuwekeza eneo hilo.

Add a comment

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola amemtaka kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Hamis Issa kurudi mkoa wa Kilimanjaro na kuhakikisha mwananchi Hemed Mbaga aliyebambikizwa kesi anatolewa mahabusu.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.