Star Tv

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu wa Gereza baada ya msamaha uliotangazwa na Rais Dk John Magufuli.


Wakili wa utetezi, Michael Ngaro anayemtetea Rugemalira amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi yanayomkabili na kwamba mpaka sasa hawajapata majibu. Kufuatia taarifa hiyo Ngaro ameuomba upande wa mashitaka kufanya mchakato ili wapate majibu ya barua hiyo haraka

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa, ni kweli wamepokea barua za washtakiwa wote wawili na kwamba zinafanyiwa kazi na watapatiwa majibu.Kutokana na kesi hiyo ambayo  ilikuja kwa ajili ya kutajwa, Hakimu Shaidi ameahirishwa hadi Oktoba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena

Seth, mwenyekiti mtendaji wa PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni mkurugenzi wa VIP wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar es Salaam, Afrika Kusini, Kenya na India.Miongoni mwa mashtaka hayo ni kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi na kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya Sh 309bilioni.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo  Juni 19, 2017 na hadi sasa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.