Star Tv

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuhamasisha Somaliland kuungana na Somalia .

Add a comment

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde. Generali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.

Add a comment
Wasichana wa shule na walimu kaskazini mashariki mwa Nigeria wamefanikiwa kukimbia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kwenye shule yao. Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi. Kusikia sauti hizo wanafunzi na walimu wao walifanikiwa kutoroka. Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok. Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana. Baada ya kupata shule ikiwa bila mtu wanamgambo hao waliipora. Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo. Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja. Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa. Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko. Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Kwa hisani ya BBC. Add a comment
Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi. Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa. Rais Muhammadu Buhari ameelezea tukio hilo kama janga la taifa. Hasira zimekuwa zikiwapanda wazazi wa wasichana hao huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa kutoka kwa vizuizi vikuu vya Dapchi mwezi uliopita. Dampchi ambao ni mji ulio kilomita 275 kaskazini magharibi wa Chibok, ulishambuliwa siku ya Jumatatu, na kusababisha wanafunzi na walimu kutoka shule moja ya serikali kukimbiliaa vichakani. Wenyeji wanasema vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiw na ndege za vita baadaye vilizima uvamizi huo. Mamlaka awali zilikana kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa, zikisema kuwa walikuw wamejificha kutoka kwa wanamgambo hao. Lakini baadaye wakakiri kuwa wasichana 110 walikuwa hawajulikani waliko baada ya uvamizi huo. Kwa hisani ya BBC. Add a comment
Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga la kitaifa. Serikali ilitoa tangazo hilo baada ya kukagua upya ukubwa na athari ya ukame huop wa miaka mitatu. Umeathiri vibaya majimbo matatu ya majimbo tisa nchini humo. Uamuzi huo umejiri wakati Cape Town umetangaza kuwa hatua za kupunguza matumizi ya maji, zinazohitaji kila raia asitumie zaidi ya lita 50 za maji kwa siku - imesaidia kuisogeza mbele "Day Zero" siku ambayo mji utakuwa hauna hata tone la maji hadi Juni 4. Limekuwa jukumu gumu kwa wakaazi wa mji huo wa Cape Town. Kima walichopewa cha lita 50 za maji kwa siku hutoshi kuoga kwa dakika chache tu na kuvuta maji chooni mtu anapokwenda haja huku mahitaji mengine kama kufua nguo mara moja kwa iki yakizangatiwa pia. Hatahivyo uamuzi wa kutangaza janga la kitaifa unamaanisha kuwa serikali kuu - inayodhibitiwa na chama tawala ANC - sasa itawajibika katika jitihada za kutoa usaidizi. Kwa mujibu wa mtandao ya wa shirika la habari eNCA, waziri wa ushirikiano nchini Des van Rooyen wiki iliopita alisema zaidi ya dola milioni 5.8 zimetengwa kukabiliana na janga hilo katika jimbo la Cape ya Magharibi, pamoja na ya Mashariki na Kaskazini, majimbo mawili ambayo hayajaangaziwa vilivyo kwenye vyombo vya habari lakini ambayo pia yanakabiliwa na athari za ukame. Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.