Star Tv
Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga la kitaifa. Serikali ilitoa tangazo hilo baada ya kukagua upya ukubwa na athari ya ukame huop wa miaka mitatu. Umeathiri vibaya majimbo matatu ya majimbo tisa nchini humo. Uamuzi huo umejiri wakati Cape Town umetangaza kuwa hatua za kupunguza matumizi ya maji, zinazohitaji kila raia asitumie zaidi ya lita 50 za maji kwa siku - imesaidia kuisogeza mbele "Day Zero" siku ambayo mji utakuwa hauna hata tone la maji hadi Juni 4. Limekuwa jukumu gumu kwa wakaazi wa mji huo wa Cape Town. Kima walichopewa cha lita 50 za maji kwa siku hutoshi kuoga kwa dakika chache tu na kuvuta maji chooni mtu anapokwenda haja huku mahitaji mengine kama kufua nguo mara moja kwa iki yakizangatiwa pia. Hatahivyo uamuzi wa kutangaza janga la kitaifa unamaanisha kuwa serikali kuu - inayodhibitiwa na chama tawala ANC - sasa itawajibika katika jitihada za kutoa usaidizi. Kwa mujibu wa mtandao ya wa shirika la habari eNCA, waziri wa ushirikiano nchini Des van Rooyen wiki iliopita alisema zaidi ya dola milioni 5.8 zimetengwa kukabiliana na janga hilo katika jimbo la Cape ya Magharibi, pamoja na ya Mashariki na Kaskazini, majimbo mawili ambayo hayajaangaziwa vilivyo kwenye vyombo vya habari lakini ambayo pia yanakabiliwa na athari za ukame.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.