Star Tv
Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi. Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa. Rais Muhammadu Buhari ameelezea tukio hilo kama janga la taifa. Hasira zimekuwa zikiwapanda wazazi wa wasichana hao huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi walikuwa wameondolewa kutoka kwa vizuizi vikuu vya Dapchi mwezi uliopita. Dampchi ambao ni mji ulio kilomita 275 kaskazini magharibi wa Chibok, ulishambuliwa siku ya Jumatatu, na kusababisha wanafunzi na walimu kutoka shule moja ya serikali kukimbiliaa vichakani. Wenyeji wanasema vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiw na ndege za vita baadaye vilizima uvamizi huo. Mamlaka awali zilikana kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa, zikisema kuwa walikuw wamejificha kutoka kwa wanamgambo hao. Lakini baadaye wakakiri kuwa wasichana 110 walikuwa hawajulikani waliko baada ya uvamizi huo. Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.