Wadau wa Uwindaji wa Kitalii wameishukuru serikali ya Marekani baada ya kuondoa zuio kwa kampuni zinazojihusisha na sekta hiyo vya kuuza Nyara za Wanyamapori hasa Simba baada ya kuthibitika kuwa sehemu ya mapato yatokanayo na uwindaji huo yanatumika vyema katika shughuli za Uhifadhi .

Serikali ya Marekani ilijiweka kando na Ununuzi wa Nyara kutoka Tanzania tangu mwaka 2014 huku Taifa hilo  likitajwa kuwa Mdau mkubwa wa Nyara hizo hasa Simba. Lakini kwa sasa milango ipo wazi ,baada ya serikali ya Marekani kuridhishwa na mwenendo wa Makampuni hayo na hii ikitokana na uwajibikaji uliofanywa na mamlaka ya usimamizi wa  wanyamapori katika kuendesha zoezi zima la Ulinzi wa Wanyamapori. Naibu Kamishna wa Utalii na Biashara kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Nchini Iman Nkui amesema, kufunguliwa kwa soko hilo kunafatiwa na ujio wa wataalam kutoka nchini Marekani kuja kuona ni jinsi gani shughuli za uwindaji zinavyosaidia Uhifadhi na Jamii. Aidha Mkui ameongeza kuwa kwa sasa Mamlaka hiyo inasubiri taarifa rasmi ya kufunguliwa kwa soko hilo ambalo litaongeza Pato la Taifa kupitia Sekta hiyo.

 

 

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.