Shirika la World Vision kanda ya Kagera limekamilisha ujenzi wa matundu nane ya vyoo,madarasa matatu ya shule hiyo , ofisi ya walimu pamoja na wodi ya mama na Mtoto katika zahanati ya kijiji cha Kiruruma kwa jumla ya thamani ya shilingi milioni mia moja sitini na tisa na kuzinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka huku meneja mradi wa World Vision.
Awali, wanafunzi zaidi ya mia nne na sabini wa shule ya Msingi Kakonje wilayani Karagwe mkoani Kagera wanatumia matundu manne ya vyoo na hivyo kujistiri katika maeneo yasiyo rasmi hali inayohatarisha mlipuko wa magonjwa miongoni mwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo.Kwa wanafunzi wa kiume ni ahueni kidogo ukilinganisha na wale wa kike ambao hujistiri kwa kuvizia kutokana na vyoo hivyo vichache kutokuwa na milango na hata ubora na hivyo kusababisha uwezekano mkubwa wa magonjwa ya mlipuko
Victor Nsiima anawataka wakazi wa maeneo hayo kuendelea na moyo wa kujitolea ili kuondoa changamoto nyingi zinazoikabili jamii hususani zilizopo katika sekta ya elimu