Star Tv

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amelitaka shirika la viwango nchini TBS na tume ya ushindani FCC kuacha kukaa ofisini badala yake wachunguze bei na uzalishwaji wa bidhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ili ziweze kupatikana kwa urahisi na kwa bei elekezi.

Add a comment

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameonya utoaji taarifa za holela na upotoshwaji kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababisha na virusi vya corona (COVID 19) unaofanywa na watu mbalimbali nchini.

Add a comment

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameaagiza shule za awali, msingi na sekondari kufungwa pamoja ratiba ya mitahani ya kidato cha sita ambao wanatakiwa kufanya mitihani tarehe 04.05.2020 na amesema ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho na wizara ya elimu.

Add a comment

Waziri  wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo  ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya,wakurugenzi na wakuu wa shule nchini,kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa usafiri kwa wanafunzi wote ambao wamekosa usafiri wa kurudi nyumbani mara baada ya shule zote kufungwa kufuatia uwepo wa ugonjwa Corona nchini.

Add a comment

Binadamu wa kwanza kufanyiwa jaribio la chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona ameanza kufanyiwa jaribio hilo nchini Marekani.

Add a comment

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la visa viwili vya wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Add a comment

Waziri wa afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amethibitisha kisa cha kwanza cha mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya Corona leo Machi 16, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Add a comment

Chama cha Mapinduzi CCM kimesitisha shughuli zenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwa ni hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

Add a comment

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo Machi 16, 2020 amefuta mbio za Mwenge kwa mwaka huu 2020 hadi pale ugonjwa wa corona utakapoisha.

Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.