Star Tv

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameaagiza shule za awali, msingi na sekondari kufungwa pamoja ratiba ya mitahani ya kidato cha sita ambao wanatakiwa kufanya mitihani tarehe 04.05.2020 na amesema ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho na wizara ya elimu.

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo Machi 17, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kubainikia kuwepo maambukizi ya homa ya virusi vya Corona  hapa nchini yaliyothitishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hapo jana Machi 16, 2020.


Waziri Mkuu amesema watu wote watakaouza vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa maambukizi ya Corona kwa bei ghali watachukuliwa hatua na serikali.
Aidha, michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile ligi kuu ya Tanzania, ligi daraja la kwanza na la pili pamoja na michezo ya shule za msingi UMITASHUMTA, UMISETA,pamoja na ile ya mashirika ya umma inayopangwa kuwepo kila mwaka kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo na kuitaka wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuwaandikia barua mashirikisho yake yote juu ya kusimamisha michezo hiyo.


Pia Waziri Mkuu amewataka Watanzania wasiokuwa na safari za lazima kwenda nje ya nchi hususani kwenye nchi zenye maambukizi kusitisha safari hizo na ametoa wito kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu maeneo yao na kuhakikisha kwamba wanafanya uchunguzi wa mara kwa mara kwa wageni wanaooneka kwenye maeneo yao na hata Watanzania wanaonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.


Watumishi wote wa mamlaka zinazosimamia uagizwaji na wageni wanaoingia  katika mipaka na viwanja vya ndege, bandari na nchi kavu wametakiwa kuendelea kusimamia kikamilifu, kufanya uchunguzi wa kiafya kikamilifu kwa kutumia vifaa ambavyo viko nchini na kuimarisha mipaka yote kwa kuhakikisha kwamba watu wote wanaoingia ndani ya nchi wanaingia kwenye mipaka rasmi.
                  Mwisho.  

Latest News

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

RAIS MAGUFULI AKABIDHI TAUSI 25 KWA MAMA MARIA NYERERE NA MARAIS WASTAAFU.
30 May 2020 09:49 - Grace Melleor

Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana I [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.