Star Tv

Waziri wa afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amethibitisha kisa cha kwanza cha mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya Corona leo Machi 16, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mgonjwa huyo ni mwanamke mwenye umri wa miaka 46 ambaye ni Mtanzania, aliyepokelewa jana nchini Machi 15, 2020 kwenye uwanja wa ndege KIA.

Waziri Ummy amesema baada ya mgonjwa huyo kupimwa jana pindi alipofika KIA hakukutwa na homa lakini baadaye alipofika hotelini alianza kujisikia vibaya na kwenda hospitalini ili kuchukuliwa vipimo ndipo alipogunduliwa tayari ana maambukizi ya virusi vya Corona na kwasasa yupo katika hospitali ya Mount Meru Arusha anaendelea vizuri na matibabu.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu Watanzania kwa kusema kuwa serikali imejiandaa kukabiliana na ugonjwa huo na inashirikiana na WHO pamoja na wadau wengine ili kutokomeza ugonjwa huo huku akiwataka wananchi  kuchukua tahadhari mapema.

Ametoa wito kwa Watanzania wasiokuwa na safari za lazima nje ya nchi kusitisha safari hizo na pia kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni pamoja na vitakasa mikono ,kuweka maji yenye dawa ya Chlorine  kwa ajili ya kusafisha mikono kwenye maeneo ya  mikusanyiko yenye watu kama vile nyumba zakulala wageni, vituo vya mabasi, na kuzitaka  hospitali za serikali na binafsi kuwekwa zuio la watu wengi  kuruhusiwa kumuona mgonjwa hospitalini.

                 Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.