Star Tv

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amelipa faini ya Shilingi milioni 70,000,000 na muda wowote kuanzia leo Ijumaa Machi 13, 2020 anatarajiwa kutoka katika gereza la Segerea.

Mbowe  ni miongoni mwa viongozi nane wa Chadema ambao pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 Milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili. 

Mbowe ambaye ni mbunge wa jimbo la Hai alihukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 70 baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka nane yakiwemo ya uchochezi.

Mpaka sasa viongozi wengine wa CHADEMA wameshatoka gerezani isipokuwa Mwenyekiti huyo wa chama Freeman Mbowe ambaye  muda wowote anatarajiwa kuachiliwa huru.

Chama hicho kimechangisha fedha kutoka kwa wanachama wake wakisaidiwa na wananchi walioguswa na hukumu ya viongozi hao ambao walihukumiwa kifungo cha miezi 5 jela au kulipa faini ya Milioni 350.

Hadi kufikia leo saa 6:00 mchana viongozi wa CHADEMA waliotoka gereza la segerea ni Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar, Salum Mwalimu; mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko,John Heche mbunge wa Tarime vijijini;Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini); mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Ester Bulaya (Bunda).

Hukumu iliyokuwa ikiwakabili viongozi hao kutoka chama cha upinzani CHADEMA ilitolewa Machi 10, 2020 ilisomwa na hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba iliyowalizimu kupelekwa gereza la Segerea hadi pale walipoanza mchakato wakulipa fedha hizo na kuanza kuruhusiwa kutoka.

                     Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.