Star Tv

Baadhi ya waombolezaji waliokuwa wakisubiri mwili wa marehemu Salome Zacharia (Mfanyakazi wa ndani jijini Arusha) nje ya hospitali ya Mount Meru wametoa maoni tofauti wakati wakizungumza na Star Tv wakisema kuwa kitendo hicho kilichofanywa na mwajiri wa binti huyo ni cha kikatili na serikali inapaswa kumchukulia  hatua za kumuwajibisha.

Salome Zacharia alifariki baada ya kuadhibiwa kwa fimbo na kufungiwa chumbani kwa muda wa siku mbili bila kupatiwa chakula na maji ya kunywa kwa kosa la kudaiwa kuiba shilingi elfu 50 hela ambayo ilikuwa ni ya muajiri wake ajulikanaye kwa jina la Mkami Shirima.

Mama mzazi wa Salome ameangua kilio katika hospitali ya Mount Meru pindi alipofika ambapo mwili wa mwanaye ulikiuwa umehifadhiwa huku akitamka maneno ya kwamba ''mwanangu ameuawa wakati hata mshahara alikuwa halipwi”.

Mwajiri aliyetenda kosa hilo tayari amekwishakumatwa na polisi na taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi mkoani Jonathan Shana amesema uchunguzi unaendelea na punde tu utakapokamilika watatoa taarifa juu ya suala hilo.

Aidha, kwa upande wake mama mdogo wa mume ambaye mke wake ndiye aliyefanya kitendo hicho amesema yeye ndiye aliyempeleka binti kwa ajili ya kufanya kazi na hivyo wazazi pamoja na walezi wa marehemu wamemtaka ahakikishe anasafirisha mwili wa mtoto wao mpaka Itigi-Singida kwa ajili ya maziko.

                        Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.