Star Tv

Binadamu wa kwanza kufanyiwa jaribio la chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona ameanza kufanyiwa jaribio hilo nchini Marekani.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington.

Wataalamu wa afya wamesema kuwa chanjo hiyo haiwezi kusababisha Covid-19 lakini ina jeni ya virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa, na uchunguzi wa chanjo hiyo utachukua miezi mingi kujua ikiwa chanjo hiyo, au utafiti mwingine, utafanikiwa.

Mtu wa kwanza kujitolea kupata dozi ya kwanza ya utafiti huo siku ya Jumatatu ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle Washington.

Aidha, inaelezwa kuwa wanasayansi kote duniani wanaharakisha utafiti wao kujaribu kupata chanjo au tiba ya coronavirus.

Na jaribio hili la kwanza kwa binadamu,lililodhaminiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani, umefanyika kando ili kuangalia kile ambacho kwa kawaida kingekua kikifanyika kuhakikisha chanjo inaweza kusababisha kuchochewa kwa kinga ya mwili katika wanyama.

Kampuni ya teknolojia ya masuala ya vimelea wa magonjwa ambayo ndiyo inayoendesha utafiti huo, Moderna Therapeutics, inasema kuwa chanjo imekwishakutengenezwa kwa kutumia mchakato uliojaribiwa na kupimwa.

Wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington, limeripoti shirika la habari la Associated Press.

Mtu wa kwanza kujitolea kupata dozi ya kwanza ya utafiti huo siku ya Jumatatu ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle Washington.

Dkt John Tregoning, mtaalamu katika magonjwa yanayoambukiza katika taasisi ya Imperial College mjini London, Uingereza,amesema: "Chanjo hii imetumia Teknolojia iliyokuwepo awali.

Amesema chanjo hiyo imefanyika kwa kiwango cha hali ya juu, kwa kutumia vitu ambavyo wanafahamu ni salama kuvitumia katika watu na wale wanaoshiriki katika jaribio hili watakuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu.

               Mwisho.

Latest News

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

RAIS MAGUFULI AKABIDHI TAUSI 25 KWA MAMA MARIA NYERERE NA MARAIS WASTAAFU.
30 May 2020 09:49 - Grace Melleor

Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana I [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.