Star Tv
Makaburi mengi mjini Dhaka, mji wenye watu wengi,ni ya muda mfupi kwa sababu, mjini Bangladesh hakuna nafasi tena ya kuzikia.Utafanya nini ikiwa mtu atachukua eneo alilozikiwa mpendwa wako? Suraya Parveen hawezi tena kutembelea kaburi la Baba yake kwasababu mwili mwingine wa mtu asiyemfahamu umezikwa kwenye kaburi hilohilo. ''Nikiwa mtoto wa kike mkubwa,nina wajibu wa kuangalia vitu.Siku moja nilimuuliza kaka yangu kama hivi karibuni alitembelea kaburi''.Aliiambia BBC mjini Dhaka. Baada ya kusita kwa muda, alimwambia kuwa kuna kaburi jingine jipya juu ya kaburi la marehemu baba yao. ''Familia nyingine sasa inamiliki kaburi hilo na wamekwishaliwekea sakafu.Taarifa hizi zimeniumiza sana, sikuweza kuzungumza kwa muda'' alieleza huku akibubujikwa na machozi.Hii si mara ya kwanza tukio hili kumtokea Suraya. Kwa mtindo huohuo alipoteza makaburi mengine ya wapendwa wake,kaburi la mtoto wake wa kwanza, Mama yake na mjomba wake. Matukio haya yamewaathiri watu wengi mjini Dhaka na kuwafanya watu kushindwa kuwa na maeneo ya kudumu ya kuwapumzisha wapendwa wao. Si kazi ngumu kupata maeneo ya kuzika, makaburi ya muda mfupi hayana gharama, lakini sheria za mji huo zinasema kila baada ya miaka miwili, mwili mwingine utazikwa kwenye eneo hilohilo. Ni hali ngumu kwa watu huko lakini hawana jinsi. Wakati mwingine wanafamilia wanazikwa kwenye kaburi moja. Kuchoma maiti haikubaliwi kwa wengi walio na imani la Kiislamu Bangladesh. Sheria za kiislamu haziruhusu kuchoma maiti katika mazishi. Tangu 2008 maafisa wa serikali wa mji wamesitisha zoezi la kugawa makaburi ya muda mrefu, wakati karburi moja la muda mfupi waweza gharamia dola za Kimarekani elfu 20, kwenye nchi yenye mapato ya mwaka ya dola za Kimarekani 1610 kwa kila mtu. Add a comment
Mwanamke mmoja kutoka nchini Ufaransa Cecile Bourgeon mwaka 2013 alidai kwamba binti yake mwenye umri wa miaka mitano Fiona alikuwa amepotea katika Hifadhi ya Clermont-Ferrand wakati akicheza na mdogo wake wa kike wa miaka 2. Jambo hilo lilizua hisia mbalimbali nchini humo lakini baada ya miezi minne ya kumtafuta mtoto huyo, Cecile na mpenzi wake Berkane Marklouf walikiri kumzika mtoto huyo msituni baada ya kutokea ajali nyumbani na mtoto huyo kufariki. Mwanamke huyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kudanganya kuhusu kupotea kwa mwanaye mwaka 2016. Hatahivyo rufaa iliyokatwa siku za hivi karibuni na kusimamiwa na jopo la Wanawake Mawakili 9 imemhukumu mwanamke huyo miaka 20 jela ikiwa ni mara nne zaidi ya kifungo cha kwanza. Add a comment
Mwanaume mmoja nchini Uingereza amekuwa agenda katika mijadala siku za hivi karibuni baada ya kukataa kabisa kujisaidia haja kubwa na hadi sasa zikiwa zimepita siku 20, akihisiwa kuwa anatembea na dawa za kulevya tumboni Polisi wanaomshikilia wameeleza kuwa wamekuwa wakimwangalia saa zote kusubiri wakati atakaojisaidia lakini bado hajafanya hivyo, lakini hata hivyo wameeleza kujipanga kwao kuendelea kumweka chini ya uangalizi wao na kusubiri hadi atakapoamua kujisaidia. Kwenye kutafuta taarifa za kidaktari kuhusu uwezekano wa mtu huyo kuhatarisha maisha yake au la kwa kitendo hicho, Shirika la Utangazaji la BBC Uingereza limezungumza na Trish Macnair, wa Primary Care Society for Gastroenterology. Trish ameeleza kuwa mwanaume huyo hatoweza kuendelea kukaa bila kujisaidia kwa muda mrefu kama anavyofikiri kwa itafika kipindi mwili utakataa kuendelea kutunza uchafu. “Utafika muda atasikia tumbo lake likisogea, japokuwa anakataa kula jambo linalofanya urahisi wa kuweza kukaa bila kwenda chooni, tumbo litaanza kusogea tu, kwani litakuwa limejaa chakula ambacho ni uchafu.” – Trish Macnair Add a comment
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini bila ya kuwepo masharti yoyote. Katika kile kinachoonekana kama kubadilska kwa mnsimamo wa Marekani, Bw Pence aliliambia gazeti la the Washington Post kuwa ikiwa Korea Kaskazini inataka mazungumzo, basi utawala wa Trump utafanya hivyo. Lakini amesisitiza kuwa vikwazo vitakuwepo hadi Korea Kaskazini ichukue hatua za kumaliza mpango wake wa silaha za nyuklia.Bw Pence alikuwa akizungumza akiwa njiani kutoka kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini, ambapo alifanya mazungumzo na Rais Moon Jae-in. Utawala wa Trump awali ulisema kuwa hautafanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un ikiwa tu yuko tayari kuachana na mpango wa nyuklia. Add a comment
Mwanamke mmoja baada ya kunywa pombe na kulewa huku wakifurahia wakati waliokuwa nao, kwenye Mji wa Bangkon nchini Thailand akiwa na rafiki yake amegongwa na kupoteza maisha huku mwenzie akijeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na treni walipokuwa wanapiga ‘selfie’. Rafiki huyo ambaye amejeruhiwa ameelezea mkasa huo na kusema walikuwa wamekunywa pombe na kulewa na ndio Marehemu akamwambia wakapige picha kwenye reli lakini hawakuwa wameona treni inayokuja upande mwingine. Tukio hilo lilitokea katika kituo cha treni cha Samsen February 8, 2018 na inaelezwa kuwa binti huyo aliyefariki alikuwa ana miaka 24 na aliumia vibaya mguu na alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitali. Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.