Star Tv
Mwanaume mmoja nchini Uingereza amekuwa agenda katika mijadala siku za hivi karibuni baada ya kukataa kabisa kujisaidia haja kubwa na hadi sasa zikiwa zimepita siku 20, akihisiwa kuwa anatembea na dawa za kulevya tumboni Polisi wanaomshikilia wameeleza kuwa wamekuwa wakimwangalia saa zote kusubiri wakati atakaojisaidia lakini bado hajafanya hivyo, lakini hata hivyo wameeleza kujipanga kwao kuendelea kumweka chini ya uangalizi wao na kusubiri hadi atakapoamua kujisaidia. Kwenye kutafuta taarifa za kidaktari kuhusu uwezekano wa mtu huyo kuhatarisha maisha yake au la kwa kitendo hicho, Shirika la Utangazaji la BBC Uingereza limezungumza na Trish Macnair, wa Primary Care Society for Gastroenterology. Trish ameeleza kuwa mwanaume huyo hatoweza kuendelea kukaa bila kujisaidia kwa muda mrefu kama anavyofikiri kwa itafika kipindi mwili utakataa kuendelea kutunza uchafu. “Utafika muda atasikia tumbo lake likisogea, japokuwa anakataa kula jambo linalofanya urahisi wa kuweza kukaa bila kwenda chooni, tumbo litaanza kusogea tu, kwani litakuwa limejaa chakula ambacho ni uchafu.” – Trish Macnair

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.