Star Tv
Maafisa wa Afya nchini Syria katika maeneo ya waasi yaliyozingirwa kaskazini mwa Ghouta wamesema watu kadhaa wamedhurika kutokana na na dalili zinazoonesha kuathiriwa na gesi ya Klorini, wakati wa mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na majeshi yanayounga mkono serikali. Taaarifa uiliyotolewa na Wizara ya Afya inayoendeshwa na wapinzani imesema waathirika, madereva wa magari ya kubeba wagonjwa na watu wengine wameripotiwa kuvuta gesi hiyo ya Klorini baada ya mlipuko. Watu 18 wanatibiwa kwa kuwekewa Oxygen. Mkazi mmoja katika eneo la mashariki ya Ghouta ameiambia BBC kuna mtoto pia ameathirika. Dokta Mohammed Khatoub aliyeko Uturuki, ambaye anatokea katika mji wa Ghouta ameelezea uthibitisho wa hospital wanakotibiwa majeruhi hao, kwamba wameathiriwa na gesi hiyo. Hata hivyo Serikali ya Syria siku zote imekuwa ikikanusha kutumia silaha za kemikali. Mashambulizi ya ardhini yalipamba moto jana Jumapili, licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusimamishwa kwa mapigano hayo. Add a comment
Mhubiri raia wa Marekani Billy Graham, mmoja wa wahubiri waliopata umaarufu mkubwa duniani katika karne ya 20 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. Graham alipata umaarufu mkubwa kama mhubiri wa kikiristo akihubiri innji sehemu mbali mbali za dunia kwenye mikutano mikubwa akianzia London mwaka 1954. Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa alikuwa amehubiria jumla ya watu milioni 210. Alianza kujitolea kuwa mkiristo akiwa na miaka 16 babada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kutakaswa kuwa mhubiri mwaka 1939. Graham ambaye alikuwa amefanya kaza kama afisa wa mauzo alikuja kuibuka kuwa muungaji mkono mkubwa wa ukiristo. Mwaka 1949 alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angels. Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi kwenye jamii nchini Marekani. Add a comment
Binadamu kwa kawaida huwa macho mchana na usiku hulala, ingawa siku hizi si ajabu kwa wengi kulala mchana na kufanya kazi usiku. Lakini je, umewahi kujiuliza mwanadamu anaweza kukaa muda gani bila kulala? Vijana wawili nchini Marekani walijaribu kupima hili. Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka wa 1963 na bendi ya Beach Boys ilikuwa ndiyo inavuma zaidi wakati huo. Marekani ilikuwa pia imeanza kujiingiza zaidi katika Vita vya Vietnam, na watoto wa shule za upili walikuwa wanajiandaa kwa likizo ya Krismasi pale vijana wawili walipoamua kufanya utafiti ambao ulilivutia taifa. Utafiti huu ulifikia kikomo mnamo 8 Januaru 1964. Randy Gardner wa miaka 17 alikuwa amefanikiwa kukaa macho bila kulala kwa siku 11 na dakika 25 mfululizo. Bruce McAllister, mmoja wa wanafunzi wa sekondari walioibuka na wazo hilo, anasema hatua hiyo ilitokana na haja ya kuunda mradi wa kuwasilisha katika maonesho ya sayansi. Baada ya kuunganisha ubunifu wao na 'utukutu' kiasi wa ujana, Bruce na rafiki yake Randy waliamua kujaribu kuvunja rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu bila kulala. Rekodi hiyo wakati huo ilikuwa inashikiwa na DJ mmoja kutoka Honolulu, Hawaii ambaye alikuwa amekaa saa 260 bila kulala (siku 10 na saa 20). "Mpango wa kwanza ulikuwa wa kuchunguza athari za kutolala kwenye uwezo wa kiajabu usioeleweka wa ubongo (ikiwa ni pamoja na nguvu za kiroho)," McAllister anasema. "Tuligundua kwamba hakukuwa na njia ya kupima hilo na kwa hivyo tuliamua kupima basi athari za ukosefu wa usingizi kwenye uwezo wa mtu kufahamu na kutambua mambo, katika kucheza mpira wa kikapu. Jambo lolote tu ambalo tungeweza." Add a comment
Kutoka nchini Syria, leo February 21, 2018 taarifa zilizoenea ni kwamba watu zaidi ya 250 wameuawa katika saa 48 zilizopita kutokana na mashambulio ya anga na silaha za ndege katika mji wa Ghouta Mashariki nchini humo. Taarifa hii imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria ambalo liko nchini Uingereza ambalo limesema idadi hiyo ya vifo inahusisha watoto 58 na wanawake 42. Shirika hilo limeeleza kuwa zaidi ya watu 1,200 wamejeruhiwa vibaya na mashumbulio hayo na kueleza kuwa takwimu hizo za vifo ni za juu zaidi tangu litokee shambulio la kemikali hapo hapo Ghouta Mashariki ambalo liliua takribani watu 1400. Add a comment
Picha ya kusisimua ya sokwe na mmoja wa waokoaji wake imeshinda tuzo la mpigapicha bora wa mwaka la Chaguo la Watu au 'People's Choice'.Picha hii iliyoshinda tuzo la mwaka ilichukuliwa na mpigapicha wa Canada, Jo-Anne McArthur ilionesha sokwe huyo mdogo, kutoka eneo la nyika Tambarale ambaye aliokolewa na kampuni ya Ape Action Africa kutoka kwa wawindaji haramu. Katika picha hii anaonekana kwenye mikono ya mchungaji wake, Appolinaire Ndohoudou, wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka kwenye makazi madogo ya sokwe hadi kwenye makao salama ya msitu wa Cameroon, ambako kuna msitu mpana zaidi. "'Ninashukuru sana kwamba picha hii imewagusa watu na ninatumai inaweza kutufundisha sote kuwajali walau kidogo wanyama," anasema McArthur. "Hakuna kitendo chochote cha ukarimu kwao kinachokua kidogo sana" "'Mara kwa mara ninarekodi ukatili wanaopitia wanyama katika mikono yetu, lakini wakati mwingine ninashuhudia taarifa za uokozi, matumaini na ukombozi wao." Picha hii ilichaguliwa takriban mara 20,000 na mashabiki wa mazingira kutoka kwenye orodha ya picha 24 zilizochaguliwa na makavazi ya kihistoria ya mali asili, ambazo zilichaguliwa kati ya picha from takriban 50,000 zilizowashilishwa kwa ajili ya shindano la kuwania tuzo la picha bora ya mwaka 2017. Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.