Morocco imesema inatumia mbinu mpya katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaotaka kuitumia kama njia ya kuingilia Ulaya, na imefanikiwa kuwazuia wahamiaji 25,000 waliojaribu kuingia Uhispania kupitia njia ya Gibraltar kwa mwaka huu pekee.
Add a commentLeo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambapo Umoja wa Mataifa umetumia siku hii kuwatunuku waandishi wawili wa shirika la habari la Reuters wanaotumikia kifungo cha miaka saba nchini Myanmar tuzo ya juu kabisa ya uhuru wa vyombo vya habari.
Add a commentRais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kulijenga upya kanisa kuu Katoliki la Notre Dame mjini Paris ambalo liliungua moto jana jioni na kusababisha uharibifu katika sehemu ya jengo hilo. Kanisa la Notre Dame lilijengwa karne ya 12 na limekuwa ni mojawapo ya vivutio vya utalii nchini Ufaransa. Kanisa hilo lilikuwa chini ya ukarabati ambao umetajwa na vyombo vya habari vya ndani kuwa chanzo cha moto. Moto huo umeunguza na kuangusha mnara wa juu wa kanisa ulio na urefu wa mita 93 ambao umekuwa ni alama ya utambulisho, lakini mkuu wa kikosi cha Zimamoto Jean-Claude Gallet amesema sehemu kubwa ya Kanisa imeweza kuokolewa baada ya maafisa kuzuia moto kuenea zaidi. Viongozi mbalimbali ulimwenguni wametuma salamu za pole kutokana na mkasa huo ambapo Kansela Angela Merkel amelielezea kanisa hilo kuwa ishara ya Ufaransa na utamaduni wa Ulaya.
CHANZO: Idhaa ya kiswahili ya DW
Add a commentSiku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]
Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]
Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]
Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.