Star Tv

Mtumishi wa kazi za ndani Ashura Suka (15) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mdogo wa mwajiri wake.

Mtoto huyo mwenye umri wa miezi 11 anadaiwa kuuawa Agosti 23, mwaka huu, saa 4:30 asubuhi, nyumbani kwa wazazi wake, Kata ya Iloganzala, Manispaa ya Ilemela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji na kueleza kuwa wanamshikilia Ashura ambaye ni mkazi wa Nyamanoro katika Manispaa ya Ilemela, akidaiwa kumuua mtoto wa mwajiri wake Kelvin Kastus mwenye umri wa miezi 11 kwa kumziba pumzi.

Ameeleza kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kutumia shuka na kusababisha kifo chake, na sasa wanaendelea na upelelezi kubaini chanzo cha mauaji hayo mara utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, Kamanda huyo wa Polisi amewataka wazazi na walezi wenye watoto wadogo kujenga utamaduni wa kuajiri watu wanaowafahamu kwa tabia, mienendo na malezi yao kwa sababu kuwaachia watu wasiowafahamu vizuri kazi ya kuwalelea watoto wadogo ni hatari.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.