Star Tv

Mkutano wa Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliokuwa akifanya na waandishi wa habari jijini Dodoma umezuiwa na polisi.

Kabla ya kuondoka katika ukumbi wa mkutano huo aliwaambia waandishi wa habari kuwa amekihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuanzi leo Aprili 28,2020 na kurudi kwenye chama alichokiasisi cha NCCR-Mageuzi.

Mbunge selasini amesema mara atakapomaliza muda wake wa ubunge na iwapo Chama hicho kitaridhia kumpokea tena ataomba wamruhusu atetee jimbo lake la Rombo kupitia NCCR-MAGEUZI.

Mkutano huo umefanyika baada ya Katibu wa mbunge wajimbo hilo Bwana Gabriel Kinabo kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa njia ya barua hapo jana juu ya uwepo wa mkutano wa mbunge Selasini na waandishi wa habari.

Mkutano huo ulibainishwa kuwa Mbunge Selasini atazungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Aprili 28, 2020 saa tano asubuhi katika Hoteli ya St. Gasper Dodoma, kwenye ukumbi wa Serengeti kuhusiana na uamuzi wa Chama chake cha CHADEMA kumtoa kwenye kundi Sogezi (WhatsaApp) ambalo amedai kundi hilo kwake ni nyenzo muhimu ya kazi na uongozi shirikishi ndani ya chama chake bila taarifa tangu tarehe Aprili 25,2020.

Joseph Roman Selasini ni mwanasiasa Mtanzania na alichaguliwa kuwa mbunge wa Rombo 2015-2020 kupitia chama cha CHADEMA.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.