Star Tv

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi ya ugonjwa huo na sasa waliopona wamefikia 48.

Waziri Ummy amesema wagonjwa hao 37 ni kati ya 108 waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona lakini sasa hawana dalili zozote za ugonjwa kama homa, mafua na kikohozi,wengine 71 wanasubiri vipimo vya mwisho na wataruhusiwa.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata maambukizi mapya kama asilimia 14.

Waziri pia ametoa wito kwa watumishi wa afya kuendelea kutoa huduma za afya kwa watu wote wanaohitaji huduma za matibabu wakiwamo wenye dalili za ugonjwa wa Corona.

Mbali na taarifa hizo za Waziri Ummy, Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la Wagonjwa wapya 15 wa corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 98 kutoka 83.

Taarifa hiyo imesema wagonjwa wote ni raia wa Tanzania ambapo wagonjwa 10 wanatoka Unguja na 05 wanatokea Pemba.

Aidha, kutokana na ongezeko la visa hivyo, mpaka kufikia sasa idadi ya visa vya corona Tanzania nzima imefikia 299 kutoka visa 284 vilivyokuwa vimeripotiwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.