Star Tv

Mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B, Assemblies of God) Dkt. Getrude Rwakatare tayari umepumzishwa katika nyumba ya milele ndani ya viunga vya kanisa hilo jijini Dar es Salaam.

Mazishi hayo yamefanyika leo Alhamisi Aprili 23, 2020, majira ya saa 7:00 mchana na kuhudhuriwa na watu wachache wa familia yake, lengo la watu hao wachache wa familia kuhudhuria  likiwa ni kuepuka mikusanyiko kama tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

Taarifa za Mama Rwakatare kufariki Dunia zilitolewa Aprili 20,2020 na mwanaye Mutta Rwakatare.

Umauti ulimkuta Mama Rwakatare katika hospitali ya Rabininsia, alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo kwa mujibu wa mwanaye Mutta  alisema kuwa Mama yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na presha.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.