Star Tv

Mamlaka ya hali hewa nchini TMA imesema hali ya muonekano wa anga kuwa na rangi nyekundu au chungwa iliyojitokeza mnamo tarehe 16 Aprili katika baadhi ya maeneo ni hali ya kawaida.

Mamlaka imetaja hali hiyo kuwa ya kawaida ambayo hutokea wakati jua linapozama au kuchomoza katika maeneo yenye hali ya hewa ambayo ina mawingu, matone madogo madogo, barafu katika anga mara tu mvua inapokatika na jua linapokuwa upande tofauti na mvua inaponyesha.


Meneja Kituo Kikuu cha utabiri ndani ya Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA, Samwel Mbuya amesema hali hiyo hutokana na miale ya jua inapokuwa imetawanywa na inapotokea hivyo kutokana na ukubwa wa matone ya maji katika wingu chembechembe mbalimbali zilizopo kwenye anga na miale ya jua hutawanywa zaidi katika mazingira ya mawimbi inayohusiana na rangi nyekundu au chungwa katika mwanga.


Aidha, Mbuya amesema hali hiyo haina tofauti na upinde wa mvua unapojitokeza angani isipokuwa katika upinde wa mvua hujitokeza rangi zote saba hivyo mabadiliko hayo hayana madhara yoyote.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.