Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania Tanzania (UNFPA na UN WOMEN) yamesaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa pamoja chini ya ufadhili wa shirika la Maesndeleo la korea KOICA.
Mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi huu Aprili 2020 hadi Machi 2023 ambao utagharimu Dola Milioni 5 za Marekani na unatarajia kuwanufaisha wanawake na wasichana 2350 wanaokumbwa na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Imeelezwa kuwa kaya 6000 zenye wanawake na wanaume wilaya ya Ikungi, Singida nao watapata nafasi ya kunufaika na mradi huo, lakini pia mradi unao mpango wa kuwafikia wananchi wapatao 40000 ndani ya mkoa wa Singida.
Mashirika hayo mawili UN Women na UNFPA yametoa wito kwa jamii kutowaacha nyuma wanawake na wasichana katika suala la kuleta maendeleo kwa kuwapatia wanawake fursa na wamelenga kuleta usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana hao hususani kwa mkoa wa Shinyanga na Singida kupitia mradi huo unaoanza kufanya kazi Aprili,2020 mpaka Machi, 2020.