Waziri wa Wizara ya Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuwepo kwa ongezeko la visa 14 vipya vya wagonjwa wa corona nchini leo Aprili 13,2010.
Waziri ummy amesema wagonjwa wote 14 ni raia wa Tanzania na mpaka kufikia sasa idadi ya watu 46 wameambukizwa virusi vya corona.
Watu 13 kati ya walioambukizwa virusi vya corona wamepatikana jijini Dar es Salaam huku mwingine mmoja akitokea jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya leo asubuhi imebainisha kuwa wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
Ikumbukwe kuwa ni jana tu Aprili 12, 2020 mamlaka ya usafiri wa anga nchini Tanzania TCAA ilitangaza marufuku ya ndege za abiria za kimataifa kutua nchini, Na tangazo hilo lilibainisha kuwa rubani na wahudumu wa ndege hizo watatakiwa kukaa karantini katika maeneo yaliyotengwa na serikali kwa gharama zao binafsi.