Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amethibitisha kifo cha mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 hapa nchini, ambaye ni Mtanzania kilichotokea alfajiri ya leo Machi 31,2020 katika kituo cha matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mlonganzila jijini Dar-es-Salaam.
Waziri Amesema marehemu ni Mtanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye mbali na ugonjwa huo alikuwa akisumbuliwa pia na maradhi mengine.
Aidha, taarifa ya Waziri Ummy imeeleza kuwa hadi kufikia leo asubuhi Machi 31, 2020 jumla ya waliopata maambukizi ya COVID-19 nchini ni 19, aliyepona ni mtu mmoja na kifo kimoja ambacho kimetokea mapema alfajiri ya leo.
Mwisho.