Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki amesema uwepo wa Reli wilayani humo utasaidia kukuza uchumi kwa wananchi pamoja na kusafirisha madini ya Gypsum.
Taarifa na Angela Mathayo
Mkuu huyo wa Wilaya ya Same ametoa kauli hiyo wakati Shirika la Reli Tanzania TRC limewasafirisha wananchi wa Wilaya ya Same zaidi ya 400 kwa kutumia usafiri wa Treni , kutoka Stesheni ya Moshi kuelekea Steseheni ya Same Mkoani Kilimanjaro,
Wananchi hao wamesafari umbali wa zaidi ya kilomita 100 wakitumia usafiri wa mabasi kutoka Wilayani Same hadi Moshi Mjini, kwa lengo la kupanda Treni ya Abiria ya Deluxe na kurejea tena Same ikiwa ni sehemu ya kutambua na kupongeza juhudi za Rais Magufuli za kurejesha usafiri huu ambao ulisimama kwa zaidi ya miaka 25.
Usafiri huo wa treni umetajwa kuwa kimbilio la wengi, ambapo hadi sasa zaidi ya abiria elfu kumi wamesafirishwa na usafiei huo tangu kurejea baada ya miaka 26.
Katika safari hiyo watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wanafunzi ,kutoka shule mbalimbali za Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Mwisho.