Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kurahisisha ulipaji wa kodi zimewezesha mapato ya kodi kwa Disemba, 2019 kuvunja rekodi na kufikia sh. trilioni 1.92.
Waziri Mkuu amesema kuimarika kwa huduma za usafirishaji na mawasiliano, upatikanaji wa huduma ya maji, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hususani makaa yam awe na dhahabu kumekuwa chachu ya mafanikio ya kuongezeka kwa mapato hayo.
Amesema kwa upande wa matumizi ya fedha kuanzia mwezi July-Disemba 2019 serikali imetumia shilingi trilioni 15.32 ambazo ni sawa 91.25% ya lengo ambapo fedha hizo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za serikali katika wizara pamoja na ugharamiaji wa deni la serikali pamoja na kazi nyinginezo.
Aidha, waziri mkuu amesema kuongezeka kwa mapato hayo kumeiwezesha serikali kuendelea kuwahudumia wananchi kupitia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa uchumi na kijamii.
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotamatishwa na mkutano wa 18 limeahirishwa leo kwa hotuba ya waziri mkuu ambayo ndani yake imetaja kuongezeka kwa mapato ya taifa.
Mwisho.