Star Tv

Wananchi  wanaoishi maeneo ya pembezoni  mkoani Arusha  wameiomba serikali kuwapelekea madaktari bingwa katika vituo vya afya vinavyojengwa katika maeneo yao ili kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu nakutumia gharama kubwa.

Taarifa na Beatrice Gelard.

Arusha ni Miongoni mwa Mikoa nchini ambayo serikali imeendelea kuboresha huduma za kijamii,zikiwemo za Afya,Elimu na Upatikanaji wa Maji safi na salama.

Moja ya miradi hiyo,ni kituo cha afya cha Muriet kilichogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Moja ambapo wakazi wa eneo hilo wanaiomba serikali kuongeza wataalam wakiwemo Madaktari Bingwa hali ambayo itawapunguzia gharama.

Kutokana na hali hiyo,Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kimefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo ya afya ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho anasema bado serikali inaendelea kuboresha Miundo mbinu hivyo wananachi hawana budi kuilinda.

Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dokta Simon Chacha amesema kituo cha Afya cha Murieti kimeendelea kuboreshwa hasa upatikanaji wa Dawa,huku Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dokta Maulid Madeni akisema Miradi mingi inajengwa kwa Mapato ya Ndani.

Chama  hicho kimetembelea miradi mbalimbali ukiwemo Ujenzi wa Mradi wa Maji, Hospitali ya Wilaya ,Ujenzi wa Madarasa ambayo yote inatarajia kuanza kufanya kazi hivi karibuni huku zaidi ya Wakazi Elfu tano wakitarajia kunufaika.

                                                                                                  Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.