Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni kitovu cha uhifadhi wa simba duniani kutokana na kuwa na wanyamapori hao wanaokadiriwa kufikia zaidi ya elfu kumi na saba ambao wamekuwa kivutio kikumbwa kwa wageni wanaoingia nchini kujionea rasilimali hiyo muhimu katika hifadhi za taifa.
Taarifa na Sadick Hunga…….
Kauli hiyo imetolewa na mtafiti kutoka katika taasisi ya utafiti wanyamapori Nchini ya Tawiri Dr. Denis Ikanda wakati alipokuwa akizungumzia suala la Simba wapatao 17 waliokuwa kifungoni katika eneo la hifadhi ya jamii la Ikona wilayani Serengeti mkoani Mara.
Dr Ikanda amesema simba hao wamepewa mafunzo maalumu ya kuwarejeshea ikolojia yao inayowawezesha kuondokana na vitendo viovu.
Aidha katika mabadiliko ya Kiikolojia kwa wanyamapori yamewezesha simba hao kupata sifa na kuondolewa katika eneo hilo ili kupelekwa katika hifadhi mpya ya taifa ya Burigi wilayi Chato mkoani Geita.
Akishuhudia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima amesema serikali itaendelea kusimamia uhifadhi ya wanyamapori katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Simba hao kumi na saba ni kati ya makundi ya simba waliokuwa katika ikolojia ya hifadhi ya taifa ya Serengeti ndani ya mapori ya akiba ya Grumet na Ikona mkoani Mara.
Mwisho.