Madereva bodaboda nchini wameonywa dhidi ya tuhuma za kujihusisha kimapenzi na wake za watu pamoja na wanafunzi zinazowakabili baadhi yao na kulitia doa kundi hilo.
Habari na Laudence Simkonda .
Inspekta Filbert Matowo ambaye ni mkaguzi wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani jiji la Mbeya, anabaisha kuwa vitendo vya baadhi ya madeleva kutembea na wake za watu vinawasababishia matatizo.
Kauli ya hii unaungwa mkono na baabdhi ya viongozi wa umoja wa madereva bodoboda ambao wameuhakikishia umma huo kuachana na vitendo vya kuwarubuni wanafunzi na hatimaye wengi wao kukatisha safari yao ya elimu..
Taasisi ya Dira women Organization, imewakutanisha vijana hambao ni madereva wanaoendesha bodaboda kwa lengo la kuwapatia elimu elekezi kwakuwa vitendo hivyo vinaelezwa kushamiri katika jamii.
Mwisho.