Wakazi wa Vijiji vya Shimbi na letu Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro wameeleza kukumbana ya upatikanaji wa huduma ya maji inayowalazimu kutembea hadi nchi jirani ya Kenya baada ya mradi wa maji unaotekelezwa kwenye eneo hilo kuchukua zaidi ya miaka saba bila kukamilika.
Habari na Rodrick Mushi
Wakizungumza mbele ya Naibu Waiziri wa maji Juma Aweso wamesema kuwa licha ya ahadi ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kuagiza mradi huo ukamilike mwezi machi mwaka jana lakini hadi sasa haujakamilika huku wananchi hao wakiendeleaa kutaabika kupata huduma ya maji..
Baada ya kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umekwama kwa miaka saba Naibu Waziri wa maji Juma Aweso ameagiza msimamizi Godson Josea na Mhandisi Amosi Thomas wanaotekeleza mradi wa maji wa kijiji cha shimbi kushikiliwa na jeshi la polisi na kuagiza kusimamishwa kuendelea na ujenzi wa mradi huo.
Wasimamizi wa mradi ambao wanashikiliwa na jeshi la polisi wametakiwa kukaa rumande hadi mkandarasi aliyepewa mradi huo atakapoonana na uongozi wa wilaya.
Mwisho