Star Tv

Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro kimeandaa mpango maalumu utakaowawezesha wahitimu wake katika chuo hicho kuweza kujiajiri na kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo.

Habari na Peter Laurence..........

Uwepo wa idadi kubwa ya wahitimu wanaomaliza elimu ya juu nchini inatajwa  kuchangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa  ajira na hivyo kupelekea vijana wengi kukosa ajira na kubaki kulalama.

Ukosefu wa misingi bora kwa wanafunzi wa elimu ya juu kunatajwa kuwa ndio chanzo cha  kushindwa kujiajiri kwa wahitmu wengi na hivyo mpango huo unasimamiwa na kitengo cha huduma za ajira chuoni hapo TESCEA   kutajwa kuwa ndio dawa ya changamoto hiyo.

Aidha, mpango mkakati uliopo kwa sasa ni kuanza kufundishwa kwa somo la ujasiriamali vyuoni ili kuweza kupunguza changamoto ya ajira kwa wahitimu.

Ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana ndio changamoto inayobainishwa na  baadhi ya  wanafunzi kuwapelekea katika msukosuko wakukosa ajira na kushindwa kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao ya elimu ya juu..

Baada ya miaka kadhaa ijayo mpango huo unatarajia kuleta majibu chanya kwa kuonyesha idadi ya wahitimu waliojiajiri huku uwajibikaji na ufanisi kwa wanafunzi hao ukitajwa kuchochea mafanikio ya mpango huo na kuweza kupunguza changamoto ya ajira.

                                                                                                   Mwisho

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.