Star Tv

Hospital ya Rufaa ya KCMC  iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro imeanza kuzalisha hewa ya oksijeni kama moja ya harakati za kukabiliana na upungufu hewa hiyo inayotumika kwa wagonjwa wenye mfumo hafifu wa upumuaji ikiwa pamoja na Watoto njiti.

Taarifa zaidi na Zephania Renatus…………

Inaelezwa kuwa teknolojia ya matumizi ya hewa ya Oksijeni katika taasisi za afya  mahala popote ulimwenguni   ni moja ya tiba muhimu hususani kwa wagonjwa wenye mfumo hafifu wa upumuaji.

Watoto waliozaliwa chini ya umri  nao wanaelezwa kuwa   wanatumia  hewa ya Oksijeni kama moja ya tiba yao ya  kuwawezesha kupumua kwa urahisi.

Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro imeazimia kumaliza tatizo la Uhaba wa hewa ya  oksijeni katika hospitali zilizopo ukanda wa kaskazini baada ya kukamilisha ujenzi wa kinu cha kuzalisha hewa hiyo.

Mhandisi wa Kinu cha kuzalisha hewa hiyo katika Hospitali ya KCMC  Danstan Kanza,amesema kinu hicho kina uwezo wa kuzalisha hadi mitungi mia nne kwa siku ,na uzalishaji huo umeanza January 13 mwaka huu.

Madaktari katika wodi ya Watoto waliozaliwa chini ya umri wamesema hewa ya Oksijeni ni moja ya tiba muhimu katika kuwawezesha watoto hao kuendelea kuishi.

Kukamilika kwa Kinu hicho sasa kunatarajiwa kumaliza changamoto ya uhaba wa Hewa ya Oksijeni kwa hospitali zilizopo ukanda wa Kaskazini hususani mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara ambapo itasaidia kutatua tatizo la upumuaji kwa wagonjwa na watoto wanaozaliwa kabla muda wao (watoto njiti).

                                                                                                                           Mwisho.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.