Naibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema wakulima wanapaswa kupimiwa maeneo yao ili kutokemeza migogoro ya ardhi nchini kwakuwa wataweza kujipatia hati miliki ya ardhi zao.
Naibu waziri huyo amebainisha hayo wakati akikabidhi hati miliki za kimila mia moja kwa wakulima wadogowadogo katika kijiji cha Litowa Mkoani Ruvuma ambazo zimetolewa na mtandao wa wakulima Mviwata kwa kushirikiana na Halmsahuri ya Wilaya ya Songea.
Mabula amesema hati hizo za kimila zilizotolewa zimelenga kutokemeza migogoro ya ardhi pamoja na kuongeza uzalishaji wenye tija
Kwa upande wake Mratibu wa MVIWATA Mkoa wa Ruvuma Laika Haji amesema utoaji wa hati hizo miliki umelenga kulinda usalama wa ardhi huku Mwenyekiti wa kijiji hicho Fabiani Shawa akiamini utolewaji wa hati hizo miliki utasaidia kukuza kilimo na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo inapoteza muda wa wakulima kuisulisha.
Zaidi ya hati za Kimila 1700 zimetolewa katika Mkoa wa Ruvuma katika wilaya za tunduru, Madaba na Songea Vijijini ambapo zaidi ya wananchi 1700 tayari wananufaika na urasimishaji huo wa ardhi.
Mwisho.