Star Tv

Vifaa vilivyokuwa  vikitumiwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA katika kuandikisha  vitambulisho vya taifa  kwenye  halmshauri ya wilaya ya Arusha iliyopo mkoani  Arusha ,vimeibiwa na watu wasiojulikana.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro ametoa siku tatu kwa watu waliohusika  na wizi huo kuvirejesha vifaa hivyo kwa hiyari mara moja  kabla ya msako msako mkali kupitia vyombo vya dola kuanza.

Muro ametoa kauli hio katika ofisi hizo za halmashauri ya Arusha ambapo  amesema baada ya siku tatu  kupita watu walioiba vifaa hivyo wasiporejesha  hatua kali itatolewa kwa yeyote atakae kutwa na kifaa chochote ambacho ni mali ya serikali.

“Namimi niseme siko tayari kuona wilaya inahujumiwa, vitu vilivyoko kwenye wilaya vinahujumiwa alafu nikakaa kimya, niwaombe wananchi mtupatie ushirikiano lakini kwa wale waliohusika tunatoa siku tatu za kujisalimisha endapo vifaa havitarudishwa kwa hiyari tutachukua hatua.”-Jerry Muro-Mkuu wa wilaya ya Arumeru.

Muro amesema vifaa vilivyoibwa ni kamera mbili, stendi mbili, kompyuta mpakato mbili, kompyuta moja aina ya Desktop, stendi mbili, Extension mbili, pamoja na keyboad.

Amewaomba wananchi kutoa taarifa pindi watakapoona mtu yeyote anauza vifaa  hivyo vilivyoibiwa na kuwataka wasinunue kamera ,kompyuta ama vitu vilivyoibwa na kuwataka  wananchi hao kutoa taarifa pindi watakapona mtu yeyote anauza vifaa hivyo .

Aidha,mesema kuibiwa kwa vifaa hivyo si mara ya kwanza kutokea kwenye ofisi za NIDA za Arumeru na  upelelezi wakubaini juu ya wizi wa vifaa hivyo unaendelea.

Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi hiyo  wameeleza hali waliyokumbana nayo baada ya kufika ofisini  na kulazimika kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

Wilson Boaz ambaye ni mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru amesema alibaini wizi wa vifaa hivyo mara tu alipofika ofisini hapo.

nilipofungua nilikuta mlango uko wazi ndipo nilitoa taarifa kwa mlinzi aliyekuwa zamu”-Wilson Boaz, Mfanyakazi wa halmashauri wilaya ya Arumeru.

Kamanda wa polisi  mkoa Arusha Jonathan Shana amethibitisha kuripotiwa tukio hilo na amesema upelelezi umeshaanza na pindi utakapokamilika  taarifa rasmi ya polisi itatolewa.

 

                                                                                                                       Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.