Star Tv

Katibu mkuu wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa Mradi wa Maji wa Mbingu Vigaeni wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro unaogharimu zaidi ya shilingi Bilion 1.5 uliotakiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 lakini mpaka sasa umefikia asilimia 15 pekee .

Mradi huo ambao alipewa mkandarasi mzawa wa kampuni ya Canopies International LTD ya Jijini Dar es salaam ambapo hadi kukamilika kwake ulipangwa kugharimu kiasi cha Shilingi Bilion 1.5 na kunufaisha wakazi wa vijiji vitatu katika Mji huu wa Ifakara.

Profesa Mkumbo amesema mkandarasi huyo anaetekeleza mradi huu anamtambua na ana miradi mingine mikubwa katika maeneo mengine nchini, hivyo uamuzi wa kuvunja mkataba ni kutaka mradi huo utekelezeke kwa wakati.

“Hatuna muda wakubembelezana na mkandarasi tuliyempa mradi lakini analeta maneno mengi na mkandarasi huyu namfahamu anayo miradi yetu mingine mikubwa huu inabidi tumnyang’anye ilia pate muda wakutekelza miradi mingine.”-Prof.Kitila Mkumbo Katibu Wizara ya Maji.

Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo anasema kinacho onekana kwenye wilaya yake ni jambo la kushangaza kwani, wamezunguukwa na mito mikubwa pamoja na uwepo wa vyanzo vya maji vya uhakika lakini kilio cha miaka yote ni uhaba wa maji.

“Wilaya hii tuna mabonde mengi yamezunguka mpaka miji lakini tunashangaa maji hayoko salama. Katika matumizi ya familia suala hili serikali imelingalia vizuri na tuna uhakika kwa maamuzi haya ambayo tumeyafikia na katibu mkuu tatizo la maji litaisha”-James Ihunyo-Mkuu wa Wilaya ya Kilombero.

Mpango wa wasimamizi wa miradi ya maji kwa wilaya hii ya Kilombero ni kuanza na utekelezaji wa maagizo ya Viongozi, sambamba na kuendelea na mikakati iliyopo katika sera ya wizara kuwa na uhakika wa maji kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa sasa upatikanaji wa maji katika mji wa Ifakara umefikia wastani wa asilimia 52 ambapo kukamilika kwa miradi iliyopangwa kutekelezwa hadi mwishoni mwa mwaka huu, kutawezesha ongezeko la upatikanaji wa maji   kufikia zaidi ya asilimia 90.

                                                                                                              Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.