Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania TCAA imewataka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kutatua changamoto ya upungufu wa marubani nchini.
Rai hiyo imetolewa wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine kuadhimisha siku ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani.
Taarifa na Adam Damian
Zoezi la kupandisha bendera ya shirika la kimataifa la usafiri wa anga duniani ICAO ambalo limetimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni ishara ya kutekeleza matawaka ya shirika hilo lililoagiza kupandishwa bendera hiyo katika mlima Kilimanjaro
Kaimu mkurugenzi mkuu TCAA Vallery Chamlungu amesema Tanzania bado haina marubani wa kutosha na kwamba mamlaka ya usafiriki wa anga imeitumia siku hiyo kuwataka wanafunzi kupenda masomo ya sayansi
Baaadhi ya wanafunzi walioshirki kwenye maadhimisho hayo wamesema watahakikisha wanafanya juu chini ili kuchangamkia fursa hiyo huku wakiishukuru TCAA kwa kuanzisha vilabu mashuleni kwani zinawasaidia kupata elimu ya masuala yanayohusu usafiri wa anga
Aidha TCAA imesema itahakikisha anga la Tanzania linaendelea kuwa salama zaidi kwa kufunga rada na mitambo ya kisasa ya kuongozea ndege sambamba na kuwasomesha wataalam wake ili waweze kuongeza ufanisi zaid katika huduma za usafiri wa anga
Katika hatua nyinge TCAA imewatunuku zawadi washindi watano wa insha iliyowataka waeleze mchango wa shirkika la ndege nchini ATCL katika uchumi wa nchi iliyowahusisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini
Maadhimisho ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani yamebeba kauli mbiu isemayo miaka 75 ya kuunganisha dunia’
Mwisho