Star Tv

Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye leo Desemba 4, 2019 ametangaza rasmi kuondoka Chama Cha Upinzani cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Akiongea leo kwenye mkutanao wake na waandishi wa Habari, Sumaye amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na mambo yasiyo mazuri ambayo yanaendelea chini kwa chini wakati alipoenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho katika ngazi ya taifa.

Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kua nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi.

Amesema alipata habari ya kuwa kanda ya Pwani kuwa kuna watu walimfuata nafasi ya uenyekiti kanda, ndipo shida ilikuja baada ya yeye kuamua kugombea nafasi nafasi hiyo ambapo lengo lake la kwanza alitaka  kubadili mitizamo kuwa ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia ya kweli

"Niliwaambia wajumbe kuwa mkifanya kama mlivyotaka kufanya, nitauthitibitishia umma kuwa ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia ya kweli, au kiti cha Mbowe kina utaratibu mwingine.

Sumaye aliendelea kuwaeleza waandishi wa habari kuwa“Nafasi ya Mwenyekiti Mbowe haiguswi mimi nilitaka kuonesha kuwa hilo sio kweli lakini nilikuwa najidanganya nimefanyiwa figisu kwenye uchaguzi wa kanda kisa niligusa kiti cha Uenyekiti Taifa.” Amesema Sumaye

“Kama wakubwa wameamua kuwashawishi wapiga kura wangu wa Kanda ya Pwani hata kwa kuwaficha Hotelini, hii maana yake naambiwa Sumaye akufukuzae akuambii toka.

Amesema baada ya kutafakari kwa kina ameona kama anaambiwa toka sasa hutakiwi isipokuwa wako watakaosikitika  lakini amelazimika kujiondoa kwny chama hicho cha upinzani( CHADEMA)

 

“Kutoka leo hii mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote najua katika kujikosha yatakuwepo maneno Kama kapewa fedha na CCM au ACT  kama nilipokuja CHADEMA nilipewa pesa basi na safari hii nimepewa fedha ingawa sijui na nani maana sijiungi na Chama chochote

Aidha Sumaye amesema kama endapo alikuja  CHADEMA kwa hiari yake basi umefika muda wa yeye kuamua kuodoka katika chama hicho,  ambapo alihamia katika chama hicho cha upinzani Agosti 25,2015.  

                                                                     Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.