Anguko la baadhi ya benki nchini limetajwa kusababishwa na masharti magumu ya uendeshaji wa taasisi za kifedha yaliyowekwa na benki kuu “BoT” likiwemo sharti la kianzio cha mtaji linalodaiwa kuzipa wakati mgumu benki za wananchi kupata leseni ya kufanya kazi.
Taarifa na Oliver Motto:-
Wanahisa wanaomiliki benki ya wananchi Mucoba PLC – wamesema kufa kwa benki nyingi za wananchi sababu ni masharti magumu yaliyowekwa na benki kuu “BoT” likiwemo sharti la benki za kijamii kuwa na mtaji usiopungua kiasi cha shilingi Bilioni mbili - jambo linalotazamwa na wanahisa kama ni miongoni mwa vikwazo kwa benki zao
Wananchi Wilayani Mufindi kwa kiwango kikubwa ndiyo wametajwa kuwa waanzilishi na wamiliki wa Benki ya wananchi Mucoba – benki ya kijamii inayoendeshwa kwa hisa za wakulima na wafanyabiashara wadogo na wakati, wananchi hao wameiomba benki ya BoT iwapunguze masharti ili benki za wananchi ziweze kuendelea.
Omary Msuya ambaye ni afisa wa benki kuu - dawati la BoT lililopo katika benki ya Mucoba, ametoa ufafanuzi juu ya hili kwa kusema kuwa.“Baada ya vitu kukaa sawa na mipangilio yote haya yote yatatatuliwa na gawio mtaweza kulipata hivyo muwe wavumilivu”.Anasema Omari Msuya
Haya yote yamezungumzwa na wanahisa katika mkutano mkuu wa 20 wa mwaka 2019 uliofanyika Mafinga Wilayani Mufindi- ambapo wanahisa walikwama kupata gawio kwa madai ya zuio lililowekwa na BoT.
Mwisho