Star Tv

Serikali imewatoa hofu wakulima wa zao la pamba kuzifanyia kazi changamoto zote zilizo jitokeza msimu wa kilimo 2018/2019 ikiwa msimu huu wa kilimo 2019/2020 changamoto hizo hazitajitokeza.

Taarifa na Mustapha  Kapalata.

Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora katika kiwanda cha kuchakata pamba Manonga Gunnery amewatoa hofu wakulima wa pamba katika msimu uliopita wa kilimo.

Naibu waziri Jaffo alisema hayo ikiwa bado mbegu za pamba hazijawafikia baadhi  ya wakulima na kuwaacha wengine  wkiendelea kulalamika juu ya ucheleweshwaji wa mbegu.

Kiwanda hiki tayari kimeanza kusambaza mbegu za pamba Tan zaidi ya 75,000 bodi ya pamba wilaya ya Igunga inathibitisha hili.Naibu Waziri Hussein Bashe ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya zinazo lima zao la hilo.

“Wakulima wa pamba wapewe mbegu kwa mkopo sio lazima walipe fedha taslimu anayetaka kulipa fedha taslimu alipe ambaye hana apewe mbegu na hili ni agizo wakuu wa wilaya wasimamie, wakuu wa mikoa wasimamie na bodi ya pamba ihakikishe mbegu zinawafikia wakulima”. Alisema Hussein Bashe.

Ilhali mbegu zinapaswa kusambazwa changamoto ya uhalibifu wa barabara ni mkubwa magari kuzama na barabara kukatika kutokana na Mvua hizi za Masika na hivyo kuwafanya baadhi wakulima wasipate mbegu kwa wakati.

 

                                                                             Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.