Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Josephat Hasunga amekabidhi ripoti ya uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya ushirika uliofanywa na Coasco katika mwaka wa fedha wa 2018/ 2019 kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Josephat Hasunga amesema ukaguzi uliofanywa katika Vyama vya Ushirika nchini humo umebaini Sh124.05 bilioni ni fedha zenye mashaka iliyotengenezwa kwa uzembe, wizi na ubadhirifu.
Amesema hayo wakati akikabidhi ripoti ya uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya ushirika uliofanywa na Coasco katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Waziri Hasunga ameikabidhi ripoti hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo ambaye amewataka waliokula fedha hizo kuanza kuzirejesha kuanzia leo kabla ya kuanza kuchukuliwa hatua.
Mwisho