Viongozi wa serikali ya Tanzania na Kenya wapo katika makubaliano ya kufanya kikao cha pamoja ili kujadili namna bora ya kuhifadhi Ikolojia ya Bonde la mto Mara kutokana na umuhimu wake katika kukuza utalii uliopo katika hifadhi ya taifa ya Serengeti na Masai Mara iliyopo nchini Kenya.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima amezungumza katika kikao cha watendaji wa bonde hilo amewataka kuzingatia umuhimu wa mto Mara unaoziunganisha nchi hizo mbili.Katika kuhakikisha suala hilo linakuwa endelevu katika nchi hizi mbili maazimio yaliyowekwa na wahasisi wa mataifa haya mawili Hayati mwalimu Julius Nyerere na Hayati Jomo Kenyata unazingatia na kupewa kipaumbele. Uhifadi wa bonde la Mto Mara umekuwa ukifanyika na nchi hizi mbili Kenya na Tanzania kutokana na umuhimu wake katika ikolojia ya viumbe hai na matumizi ya kibinaadam waliopo pembezoni mwake.