Baadhi ya wakulima wa Pamba Wilayani Sengerema mkoani Mwanza , wamesema kukosena kwa mnunuzi wa zao la Pamba tangu msimu ulipofunguliwa umesababisha maisha kuwa ghalikutokana na ukosefu wa fedha. Wananchi wa kijiji cha Lugongo kata ya Kasenyi wamseama mpaka sasa hawajapata ufumbuzi juu ya malipo yao ya mauzo ya Pamba licha ya viongozi wanauhuska katika malipo wakitoa ahadi kila kukicha
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha wakulima wa pamba katika kijiji cha lugongo Alex Mahilane amesema amekusanya tani 68 za pamba na zimeifadhiwa kwenye ghala zikiwa na thamani ya shilingi Milion 81.6 ambapo kati ya fedha hizo hakuna pesa ambayo imeshalipwa kwa wauzaji wa zao hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole akitolea ufafanuzi suala hilo amesema kuwa wilaya ya Sengerema mpaka sasa haijapata mnunuzi ambapo amewataka wakulima kuwa na subra wakati serikali ikiendelea kulitafutia ufumbuzi suala hilo.