Star Tv

Serikali imeamua kutekeleza mikakati mbalimbali yenye lengo la kuleta maendeleo kwa nchi ikiwemo sekta ya mifugo kwa lengo la kupunguza magonjwa kwa wafugaji na kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama kwa kupanda malisho. Wilaya zilizotembelewa ni pamoja na Maswa, bariadi pamoja na vijiji, katika mkoa wa Simiyu.

 Malisho yamekuwa ni moja ya changamato kwa wafugaji kutokana na ukosefu wa maeneo ya kuchungia jambO ambalo limekuwa likileta migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini. Vilevile changamoto hiyo imekuwa ikishangia mifugo kukosa afya kwakutopata malisho bora yenye vitamini na wanga hali inayopelekea mifugo kukabiliwa na magonjwa.

 Dk; Angelo Mwilawa ambaye ni mkurugenzi wa utafiti, mafunzo na ugani kutoka wizara ya mifugo na uvuvi amebainisha hayo wakati akitoa mafunzo ya uvunaji wa mbegu na uhifadhi wa malisho ya mifugo kwa njia ya hei (nyasi zilizokaushwa). Yaani nyasi zilizovunwa na kunyaushwa zikiwa na ubora wa virutubisho kwa mifugo.

 Huu ni mkakati na mpango endelevu, wa kuendeleza ufugaji bora na wenye tija kwa wafugajiwizara hii ya mifugo na uvuvi ikiwa chini ya Waziri Luhaga Mpina.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.