Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima mbegu ili kunusuru zao la Alizeti kutokana na kiwanda cha kuongeza thamani ya zao hilo kukosa malighafi.
Serikali imewataka wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda nchini ili viweze kuongeza thamani ya mazao toka mashambani. Kiwanda cha kuchenjulia mafuta ya Alizeti cha Mossegi kilichopo wilayani Serengeti mkoani Mara kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa malighafi hatua inayoelezwa kuwatia hasara wawekezaji. Pamoja na tatizo hilo lakini pia kiwanda hicho kinatatizo la kukatika umeme mara kwa mara suala linalofanya gharama za uendeshaji kuwa juu katika uendeshaji wake.
Kutokana na hali hiyo halmashauri ya wilaya ya Serengeti imetenga fedha zaidi ya shilling miilioni ishirini na tano ili kuweza kunusuru hali hiyo kwa kuwagawia mbegu wakulima.