Serikali imeamua kuanza kutekeleza miradi ya maji nchini kupitia mamlaka za maji za mikoa baada ya miradi hiyo iliyokuwa ikijengwa na makandarasi kuchukua muda mrefu bila kukamilika.
Waziri wa maji profesa Makame Mbarawa ametangaza uamzi huo wakati akiikabidhi MWAUSWA mradi wa maji ulioko kata ya Kikubiji katika wilaya ya Kwimba jijini Mwanza uliotumia miaka sita bila kukamilika.
Ameeleza kuwa matatizo ya maji katika maeneo mengi nchini yamesababishwa na baadhi ya makandarasi na wataalamu wasio waadilifu. Baada ya kukabidhiwa mradi huo mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jijini mwanza MWAUWASA mhandis Anthon Sanga ameahidi kuwa mamlaka yake itajitahidi kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ndani ya siku sitini. Awali akitoa taarifa ya mradi huo mhandisi wa maji wilayani kwimba Boaz Pius amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza tangu mwaka 2013 na ikiwa utakamilika baada ya kukabidhiwa MWAUWASA unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi elfu kumi na sita.