Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, ameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kutumia vyakula, vipodozi na dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi. Ilikuwa ni kikwazo kwa wajasiriamali wadogo mkoani Simiyu kufuata huduma za Mamlaka ya Chakula Dawa TFDA jijini Mwanza, lakini kwa sasa wamesogezewa huduma karibu mjini Bariadi, pamoja na kupongeza hatua hii, changamoto hazikosekani.
TFDA imezindua ofisi mjini Bariadi kwa ajili kusogeza huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki ambayo ni Simiyu, Mara na Shinyanga, ambapo Kaimu Meneja wa Kanda hiyo Nuru Mwasuluma anaelezea namna walivyojipanga kutoa huduma, kubwa kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, vipodozi na dawa.
Aidha Mtaka amesisitiza mamlaka hiyo kuangazia zaidi maeneo ya vijijini ambayo kwa muda mrefu yamesahaulika, huku wananchi wakiwa kwenye hatari ya kuuziwa na kutumia bidhaa zilizomaliza muda wake wa matumizi.