Star Tv

Baraza la Habari Tanzania, Latangaza majina ya wateule wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari, EJAT kwa mwaka 2018-2019 ambapo idadi hiyo imeongezeka kufikia wateule 81 ikiwa ni ongezeko la wateule 27 ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo ilikuwa wateule 57. Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2018 kunafuatia kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi uliofanywa na jopo la majaji saba lililokaa kuanzia june 13 hadi 19 mwaka huu. Sahara Media Group ikiongozwa na waandishi  ambao ni Kisali Simba, Projestus Binamungu na Salma Mrisho amboo ni kati ya wateule wa tuzo hizi.

Jumla ya Kazi za kiuandishi 644 zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa ishirini kwenye tuzo hizo ambapo kuna ongezeko la wateule kwa upande wa luninga wateule 20 kutoka
15,redio wateule 20 kutoka 11, magazeti wateule 46 kutoka 19 na ushiriki wa wanawake umeongezeka kufikia wateule 34 kutoka 24 kwa mwaka 2017.
Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji Baraza la Habari MCT ameelezea changamoto kubwa iliyojitokeza katika kuzipitia kazi mbalimbali ni Waandishi wa habari
kuandika habari ambazo hazina muendelezo pamoja na kutumia chanzo cha habari kimoja. Tuzo hizo zitatolewa juni 29 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa

Profesa Chriss Maina Peter Mtaalamu wa Sheria kutoka Chuo Kkikuu cha Dar es salaam na Mchambuzi wa masuala ya siasa na uhuru wa kujieleza.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.