Wilaya ya Bukombe imetoa maazimio kwa wanunuzi wa pamba kuwa ifikapo juni 24 Kampuni itakayoshindwa kununua vituo vyake vitakabidhiwa kwa kampuni zitakazokuwa zimeanza ununuza wa Pamba wani Halmashauri haiko tayari kuona ikipoteza mapato.
Baada ya kuibuka kwa mjadala wa Wakulima kutorosha pamba usiku na kwenda kuuza Chato kutokana na wanunuzi kutoanza kununua tangu msimu uanze mwezi Mei. Makampuni Manne yaloingia mkataba na Halmashauri yameeleza sababu kubwa ya kukwama ni anguko la bei solo la dunia.
Ahadi waliyoiweka wanunuzi ni kuwa jumatatu ijayo wataanza zoezi la ununuzi wa pamba. Wilaya ilihamasisha Wakulima walime zao la pamba na muitikio ulikua mkubwa. Hali ya kuchelewa kuuzwa kwa pamba imesababisha baadhi ya wakulima kuuza kwa bei ya chini wasipate athari huku bei elekezi ya 1200. Makampuni yametakiwa kutii maagizo yaliyotolewaPamoja na hayo makampuni yameomba sasa Wilaya idhibiti utoroshaji wa Pamba usiendelee.